• HABARI MPYA

  Thursday, January 01, 2015

  SONY SUGAR YASHUSHA VIFAA VINNE AWENDO

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  KLABU ya ligi kuu ya taifa la Kenya, SoNy Sugar imewasajili wachezaji wanne katika dirisha refu la uhamisho linaloendelea nchini Kenya.
  Miongoni mwa vifaa vipya ni makipa wawili Jairus Adira ambaye alituzwa kipa bora wa msimu 2014 na Kevin Omondi kutoka Chemelil Sugar na Nairobi City Stars mtawalia. Kinda Omondi kwa upande wake alimaliza wa pili kwenye tuzo za wachezaji chipukizi msimu wa 2014.
  Kando na wawili hao, vijana hao wa kocha Zedekiah Zico Otieno pia wamezinasa huduma za beki David Mwangi kutoka Mathare United na kiungo mshambulizi Vincent Ogutu kutokea Kakamega Home Boyz.
  Jairus Adira akipokea tuzo ya kipa bora msimu uliopita

  “Tumemaliza kuwasajili wachezaji wanne; David Mwangi kutoka Mathare United, Vincent Ogutu wa Kakamega Homeboyz, Jairus Adira kutoka Chemelil Sugar na Kevin Omondi wa Nairobi City Stars,” meneja wa timu Stock Ouma alithibitishia BIN ZUBEIRY.
  Adira na Omondi wametia wino kwenye mkataba wa miaka mitano huku Mwangi na Ogutu wakisaini mikataba ya miaka mitatu na minne katika usanjari huo.
  Hizi ni habari njema kwa klabu hiyo iliyoko Awendo, magharibi mwa Kenya iliyowatema wachezaji sita; waganda Ronny Kagunzi na John Bosco Ssemugenyi, Patrick Kennedy Otieno, Anthony Odinga, Antony Andrew na Joseck Gathongo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SONY SUGAR YASHUSHA VIFAA VINNE AWENDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top