• HABARI MPYA

  Thursday, January 08, 2015

  AKINA TORRES WAIZAMISHA REAL MADRID 2-0 KOMBE LA MFALME

  TIMU ya Real Madrid imefungwa mabao 2-0 na wenyeji Atletico Madrid katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Mfalme, maarufu kama Copa del Rey Uwanja wa Vicente Calderon usiku huu.
  Mshambuliaji Fernando Torres aliichezea kwa mara ya kwanza klabu yake ya zamani, Atletico baada ya kurejea wakati Cristiano Ronaldo alianzia benchi kwa maumivu ya goti kabla ya kuingia kipindi cha pili.
  Winga Gareth Bale aliifungia bao Real mapema, lakini likakataliwa kwa sababu alikuwa ameotea, kabla ya Raul Garcia kuifungia bao la kwanza Atletico dakika ya 58 kwa mkwaju wa penalti kufuatia yeye mwenyewe kuangushwa na Sergio Ramos.
  Jose Gimenez akamfurahisha zaidi kocha wake Diego Simeone kwa kufunga bao la pili dakika ya 76. Mchezo wa marudiano utachezwa Uwanja wa Bernabeu Alhamisi ya Januari 15 na Real wanatakiwa kushinda 3-0 ili kutinga Robo Fainali.  
  Kikosi cha Atletico Madrid kilikuwa; Oblak, Gamez, Godin, Gimenez, Lucas, Mario, Gabi, Saul/Turan, Raul Garcia, Griezmann/Mandzukic na Torres/Koke.  
  Real Madrid; Navas, Arbeloa/Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo, Kroos, Khedira, Bale, Isco, James/Ronaldo na Benzema/Jese.
  Atletico Madrid midfielder Raul Garcia (right) wheels away after opening the scoring with a second half penalty
  Mshambuliaji wa Atletico, Fernando Torres (kushoto) akikimbia na mfungaji wa bao lao la kwanza, Raul Garcia (kulia) kushangilia

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2901036/Atletico-Madrid-2-0-Real-Madrid-Raul-Garcia-Jose-Gimenez-strike-gain-upper-hand-Copa-del-Rey.html#ixzz3OAxrrUOg 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AKINA TORRES WAIZAMISHA REAL MADRID 2-0 KOMBE LA MFALME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top