• HABARI MPYA

  Wednesday, January 07, 2015

  MWADUI YABANWA NA JKT OLJORO, SARE 2-2

  Bakari Kigodeko ameifungia Mwadui leo 
  Na Philipo Chim, SHINYANGA
  WENYEJI, Mwadui wamelazimishwa ya kufungana mabao 2-2 na JKT Oljoro katika mchezo wa Kundi B, Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara jioni ya leo.
  Mabao ya Mwadui yalifungwa na Razack Khalfan dakika ya 17 kwa penalti, baada ya beki Bakari Mikidadi wa JKT Oljoro kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, wakati la pili lilifungwa na Bakari Kigodeko dakika ya 60.
  Mabao ya JKT Oljoro yalifungwa na Saleh Hussein dakika ya 13 na Sino Augustino dakika ya 80.
  Mwadui inatimiza pointi 29 na kuzidi kung’ara kileleni, wakati JKT Oljoro wapo nafasi ya tatu nyuma ya Toto Africans kwa pointi zao 24.
  Katika mechi nyingine za ligi hiyo leo, Ashanti United imetoka sare ya 2-2 na Kurugenzi ya Mafinga, wakati Burkina Faso imeifunga 4-1 Polisi Mara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWADUI YABANWA NA JKT OLJORO, SARE 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top