• HABARI MPYA

    Friday, June 02, 2023

    WAZIRI DKT. CHANA AZURU KAMBI YA YANGA ALGERIA AITAKIA HERI


    WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana leo amewasili katika  Ubalozi wa Tanzania ulioko Jijini Algiers nchini Algeria na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu ikiwa ni maandalizi ya kushuhudia mchezo wa Fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na wenyeji, USM Alger kesho.
    Mara baada ya kuwasili katika Ubalozi huo, Balozi Dkt. Pindi Chana amesaini Kitabu cha Wageni pamoja na kuzungumza na Balozi wa Tanzania nchini humo pamoja na kupata nafasi ya kuzungumza na wachezaji wa Timu ya Yanga katika Kambi yao, ambapo mbali na kuwatakia heri, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. ameahidi zawadi zaidi endapo watabeba Kombe na Watanzania wanawaombea na kuwatakia heri pia.
    Katika ziara hiyo Chana ameambata na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tabia Maulid, Mwenyekiti UWT Taifa, Mary Chatanda, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Nicholas Mkapa, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, baadhi ya  Waheshimiwa Wabunge na mashabiki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI DKT. CHANA AZURU KAMBI YA YANGA ALGERIA AITAKIA HERI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top