• HABARI MPYA

  Monday, June 12, 2023

  NI AHLY MABINGWA WA AFRIKA KWA MARA YA 11


  TIMU ya Al Ahly SC ya Misri imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya sare ya 1-1 na wenyeji Wydad Athletic Club waliokuwa pia wanashikilia taji hilo usiku wa jana Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
  Wydad walitangulia na bao la beki wake, Yahya Attiat-Allah El Idrissi dakika ya 27, kabla ya Mohamed Abdelmonem kuisawazishia Al Ahly dakika ya 78.
  Al Ahly wanabeba Kombe kwa ushindi wa jumla wa 3-2, kufuatia kuwachapa Wydad 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Jijini Cairo na hilo linakuwa taji la 11 jumla kwao wakiendelea kuwa washindi wa mataji hayo mengi zaidi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI AHLY MABINGWA WA AFRIKA KWA MARA YA 11 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top