• HABARI MPYA

  Sunday, June 18, 2023

  CHAMA AISHUHUDIA ZAMBIA IKIKATA TIKETI YA AFCON NDOLA

  KIUNGO wa Simba, Clatous Chama jana alikuwa benchi muda wote kuishuhudia timu yake ya taifa, Zambia ikikata tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Ivory Coast baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji wa fainali hizo, Tembo Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola.
  Mabao ya Chipolopolo yalifungwa na Serge Aurier aliyejifunga dakika ya 31, Patson Daka dakika ya 48 na Kings Kangwa dakika ya 55 na kwa ushindi huo kikosi cha Avram Grant kinafikisha pointi 12, mbili Zaidi ya Ivory Coast na zote zimefuzu AFCON zikiziacha Comoro yenye ponti sita na Lesotho pointi moja kuelekea mechi za mwisho za Kundi H.
  Mabingwa hao wa mwak 2012, Zambia wanafuzu AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2015 wakitoka kukosa kukosa Fainali tatu zilizopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHAMA AISHUHUDIA ZAMBIA IKIKATA TIKETI YA AFCON NDOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top