MABINGWA watetezi, Mtibwa Sugar wamepangwa Kundi A katika Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 inayotarajiwa kuanza Juni 21 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Katika Kundi hilo, A Mtibwa Sugar ya Morogoro ipo pamoja na Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani, Mbeya City ya Mbeya na Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi.
Kundi B linaundwa na Yanga SC ya Dar es Salaam, Polisi Tanzania ya Kilimanjaro, Dodoma Jiji ya Dodoma na Tanzania Prisons ya Mbeya, wakati Kundi C kuna Coastal Union ya Tanga, Geita Gold ya Geita, Singida Big Stars ya Singida na KMC ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Kundi D linawakutanisha Simba SC na Azam FC zote za Dar es Salaam, Ihefu SC ya Mbarali mkoani Mbeya na Kagera Sugar ya Bukoba.
0 comments:
Post a Comment