• HABARI MPYA

  Sunday, June 18, 2023

  RAIS WA ZANZIBAR DK. HUSSEIN MWINYI AITAKIA HERI TIMU YA OLIMPIKI MAALUM


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi ameitakia kila la heri Timu ya Olimpiki Maalumu itakayoshiriki Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalum (Special Olympics World Games) nchini Ujerumani.
  Mhe. Mwinyi amekutana na timu hiyo leo Juni 17, 2023 Jijini Berlin wakati wa hafla ya chakula cha mchana aliyowaandalia wachezaji na Viongozi wa timu hiyo iliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani.
  Amewatia moyo na kuwatakia kila kheri katika mashindano hayo pamoja na kuwaalika Zanzibar pindi watakapomaliza mashindano.
  Rais Dk.Mwinyi atahudhuria ufunguzi wa Mashindano ya Olimpiki Maalumu ya Dunia yanayotarajiwa kufunguliwa leo tarehe 17 Juni hadi 25 Juni katika uwanja wa Olimpia Berlin, Ujerumani, ambapo wanamichezo zaidi ya 7000 kutoka nchi 190 wanatarajia kushiriki.
  Wakati wa hafla hiyo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alimuahakikishia Mhe. Rais Mwinyi kuwa maandalizi ya timu ya Olimpiki Maalam kushiriki mashindano ya mwaka huu yanaenda vizuri na wachezaji wako katika hali nzuri.
  Mwaka 2019 Tanzania iliibuka mshindi wa Dunia katika mchezo wa Mpira wa Wavu na kwa upande wa riadha iliibuka na medali ya shaba kwenye michezo iliyofanyika Abu Dhabi, UAE.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS WA ZANZIBAR DK. HUSSEIN MWINYI AITAKIA HERI TIMU YA OLIMPIKI MAALUM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top