• HABARI MPYA

  Saturday, June 24, 2023

  MASHUJAA WAIPIGA TENA MBEYA CITY PALE PALE SOKOINE NA KUPANDA LIGI KUU


  TIMU ya Mashujaa ya Kigoma imefanikiwa kupanda Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa marudiano wa Mchujo wa kuwania kucheza ligi hiyo msimu ujao uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Bao pekee la Mashujaa leo limefungwa na John Budeba dakika ya 87 na kwa kwa matokeo hayo wanapanda kwa ushindi wa jumla wa 4-1 kufuatia kushinda 3-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma wiki iliyopita.
  Mashujaa walifikia hatua hii baada ya kuwatoa Pamba FC ya Mwanza waliokuwa nao Championship, wakati Mbeya City iliangukia hapo baada ya kutolewa na KMC waliokuwa nao Ligi Kuu katika mechi za mchujo wa kwanza.
  Hii inamaanisha msimu ujao kutakuwa na wageni watatu kutoka Championship, mbali na Mshujaa nyingine ni mabingwa JKT Tanzania na washindi wa pili, KITAYOSCE ya Tabora, wakati timu tatu zimeshuka kutoka Ligi Kuu, pamoja na Mbeya City ni Ruvu Shooting na Polisi Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHUJAA WAIPIGA TENA MBEYA CITY PALE PALE SOKOINE NA KUPANDA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top