• HABARI MPYA

  Thursday, June 15, 2023

  AZAM FC PANGA LAHAMIA KWA WACHEZAJI WAZAWA


  KLABU ya Azam FC imeendelea kupiga panga wachezaji na leo imehamia kwa wachezaji wazawa, ikitangaza kuwaacha Ismail Aziz Kader na Cleophace Mkandala.
  Wawili hao wanafanya idadi ya jumla ya wachezaji walioachwa kufika watano, baada ya jana kuwaacha 
  beki Mzimbabwe Bruce Kangwa, kiungo Mkenya, Kenneth Muguna na mshambuliaji Mzambia, Rodgers Kola.
  Azam FC pia imeachana na makocha wake wawili, Kocha wa makipa Mspaniola Dani Cadena na kocha wa Fiziki, Mtunisia Dk. Moadh Hiraoui.
  Makocha hao wanaondoka kupisha wasaidizi wapya watanaoletwa na kocha mpya, Msenegal Youssouph Dabo ambaye ataanza kukiandaa kikosi kwa ajili ya msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC PANGA LAHAMIA KWA WACHEZAJI WAZAWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top