• HABARI MPYA

  Friday, June 09, 2023

  KMC NA MBEYA CITY KUMALIZANA KATIKA PLAY-OFF


  TIMU za Mbeya City na KMC zitamenyana katika mechi mbili za nyumbani na ugenini kuwania kubaki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
  Hiyo ni baada ya KMC kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City, bao pekee la Deogratius Kulwa dakika ya kwanza tu katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu leo Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Kwa matokeo hayo, KMC inamaliza nafasi ya 13 kwa pointi zake 32, moja zaidi ya Mbeya City iliyomaliza nafasi ya 14 na zitamenyana wiki ijayo katika mechi mbili za nyumbani na ugenini, timu itakayoshinda itabaki Ligi Kuu.
  Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na Mashujaa FC kutoka Championship katika mechi nyingine mbili za nyumbani na ugenini kuwania kurejea Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC NA MBEYA CITY KUMALIZANA KATIKA PLAY-OFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top