• HABARI MPYA

  Wednesday, June 21, 2023

  YANGA YAACHANA NA ‘TOTO TUNDU’ BERNARD MORRISON


  KLABU ya Yanga imetangaza kuachana na winga Mghana, Bernard Morrison baada ya msimu mmoja tangu arejee kutoka kwa mahasimu, Simba SC.
  “Tunamshukuru Morrison kwa mchango wake katika kipindi chote alichokuwa nasi na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya nje ya Young Africans SC,”imesema taarifa ya Yanga usiku huu.
  Morrison alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza katika dirisha dogo mwaka 2020 akitokea DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mwishoni mwa msimu akahamia kwa mahasimu, Simba ambako alicheza hadi Julai mwaka jana aliporejea Jangwani.
  Bernard Morrison anakuwa mchezaji wa nne kuondoka baada ya kiungo Mzanzibari Feisal Salum aliyeuzwa Azam FC, mawinga wengine, Mkongo Tuisila Kisinda na mzawa, Dickson Ambundo.
  Tayari Yanga imeachana na Kocha wake Mkuu, Mtunisia Nasredeen Nabi na Kocha wa makipa, Mbrazil Milton Nienov.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAACHANA NA ‘TOTO TUNDU’ BERNARD MORRISON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top