• HABARI MPYA

    Monday, June 12, 2023

    KOCHA NABI AMSHUKURU RAIS DK SAMIA SULUHU HASSAN MAFANIKIO YA YANGA

    KOCHA Mtunisia wa Yanga, Nasredine Mohamed Nabi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake kwenye klabu hiyo na sekta ya michezo kwa ujumla.
    Nabi amesema hayo baada ya mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
    Shujaa wa Yanga leo ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Kennedy Musonda aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 14 akimalizia kazi nzuri ya beki Mkongo, Djuma Shabani.
    Pamoja na ubingwa wa Ligi Kuu na ASFC, Yanga pia ni washindi wa Ngao ya Jamii na washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika, wakihitimisha msimu mzuri kwao kihistoria chini ya kocha Nabi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA NABI AMSHUKURU RAIS DK SAMIA SULUHU HASSAN MAFANIKIO YA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top