• HABARI MPYA

  Monday, June 26, 2023

  MTIBWA, GEITA GOLD ZATINGA ROBO FAINALI LIGI YA U20


  MABINGWA watetezi, Mtibwa Sugar wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Ligi ya Vijana U20 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Said Mkopi na Samuel Mbigiri, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Samson Joseph.
  Mechi nyingine ya Kundi A jana Mbeya City iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Namungo FC, wakati mechi za Kundi KMC iliichapa Singida Big Stars 3-0 na Geita Gold ikailaza Coastal Unión 1-0.
  Kwa matokeo hayo Mbeya City inaungana na Mtibwa Sugar kutoka Kundi A kwenda Robo Fainali, wakati kutoka Kundi C Geita Gold wamefuzu kama vinara kwa pointi zao tisa wakifuatiwa na Coastal Union waliomaliza na pointi sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA, GEITA GOLD ZATINGA ROBO FAINALI LIGI YA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top