KATIKA kutekeleza agizo la kikanuni la leseni za vilabu kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Azam FC imeingia makubaliano ya ushirikiano na klabu ya wanawake ya Baobab Queens ya Dodoma.
Kwa mujibu wa kanuni mpya za CAF, klabu yoyote itakayopata nafasi ya kushiriki mashindano ya Afrika kuanzia msimu wa 2023/24, itapaswa aidha kuwa na timu ya wanawake au kushirikiana katika uendeshaji na taasisi nyingine yenye timu ya wanawake.
Kwa makubaliano hayo na Baobab, ni rasmi sasa kwamba klabu hiyo ya Dodoma itakuwa klabu dada ya Azam FC kuanzia msimu ujao.
Baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Azam FC itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment