• HABARI MPYA

  Friday, June 16, 2023

  KMC BADO WAPO WAPO SANA LIGI KUU, WAIPIGA MBEYA CITY 2-0 UHURU


  TIMU ya KMC ya Kinondoni imefanikiwa kusalia Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya City jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya KMC katika mchezo huo wa marudiano wa mchujo wa kukwepa kuteremka daraja yamefungwa na Daruwesh Saliboko dakika ya tatu na Awesu Awesu dakika ya 28.
  KMC inabaki Ligi Kuu kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumanne Jijini Mbeya na sasa Mbeya City itakwenda kumenyana na Mashujaa ya Kigoma kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC BADO WAPO WAPO SANA LIGI KUU, WAIPIGA MBEYA CITY 2-0 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top