• HABARI MPYA

  Wednesday, June 21, 2023

  SIMBA SC YAMUACHA NELSON OKWA ILIYEMTOA RIVERS UNITED


  KLABU ya Simba imeachana na kiungo mshambuliaji Mnigeria, Nelson Esor-Bulunwo Okwa baada ya msimu mmoja tangu asajiliwe kutoka Rivers United ya kwao.
  Pamoja na kusajiliwa mwanzoni mwa msimu, lakini Okwa alipelekwa kwa mkopo Ihefu SC ya Mbeya ambako alimalizia msimu.
  Anakuwa mchezaji wa nne kuonyeshwa mlango wa kutokea Simba baada ya beki Muivory Coast, Mohamed Ouattara, kiungo Mnigeria Víctor Akpan na winga Mghana, Augustine Okrah.
  Simba pia imeachana na makocha wake wawili wa Fiziki, Kelvin Mandla Ndlomo na Fareed Cassiem, wote raia wa Afrika Kusini na kocha wa makipa, Mmorocco, Zakaria Chlouha na kocha wake wa timu yake ya wanawake, Mganda Charles Lukula.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMUACHA NELSON OKWA ILIYEMTOA RIVERS UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top