• HABARI MPYA

  Friday, June 02, 2023

  SAKHO AITWA TIMU YA TAIFA SENEGAL KUIVAA BRAZIL


  KOCHA wa Senegal, Aliou Cissé  amemjumuisha kwenye kikosi chake winga wa Simba SC, Pape Ousmane Sakho kwa ajili ya mbili mwezi huu dhidi ya Benín Juni 17 na Brazil Juni 20 zote ugenini.
  Mechi dhidi ya Benín ni ya Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani ambazo wao Ivory Coast ndio wenyeji na ya Brazil ni ya kirafiki ambayo itapigwa Uwanja wa José Alvalade Jijini Lisbon nchini Ureno.
  Senegal imekwishajihakikishia tiketi ya AFCON ya mwakani ikiwa inaongoza Kundi L kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na Msumbiji pointi nne, Rwanda tatu na Benín mbili kuelekea mechi mbili za mwisho.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAKHO AITWA TIMU YA TAIFA SENEGAL KUIVAA BRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top