• HABARI MPYA

  Saturday, June 17, 2023

  PANGA LAENDELEA AZAM FC, KIPA MASEKE NAYE ATEMWA

  KIPA chipukizi, Wilbol Maseke Changarawe amekuwa mchezaji wa sita kutemwa kwenye kikosi cha Azam FC baada ya kumalizika kwa msimu wa 2022-2023.
  Maseke anaungana na beki Mzimbabwe Bruce Kangwa, kiungo Mkenya, Kenneth Muguna na mshambuliaji Mzambia, Rodgers Kola na wazawa wenzake, Ismail Aziz na Cleophace Mkandala.
  "Ahsante sana kwa kumbukumbu zako ndani ya klabu yetu, ulianzia kwenye kituo chetu cha kukuza vipaji 'Azam FC Academy', kabla ya kupandishwa timu kubwa 2019. Tunakutakia kila la kheri kwenye maisha yako mapya ya soka," imesema taarifa ya Azam FC.
  Pamoja na wachezaji hao, Azam FC pia imeachana na makocha wake wanne, aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu, Kali Ongala, Msaidizi wake, Aggrey Morris, Kocha wa Makipa, Mspaniola Dani Cadena na kocha wa Fiziki, Mtunisia Dk. Moadh Hiraoui.
  Makocha hao wanaondoka kupisha wasaidizi wapya watakaoletwa na kocha mpya, Msenegal Youssouph Dabo ambaye ataanza kukiandaa kikosi kwa ajili ya msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PANGA LAENDELEA AZAM FC, KIPA MASEKE NAYE ATEMWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top