• HABARI MPYA

  Monday, June 19, 2023

  MAYELE ATOKEA BENCHI KUIFUNGIA DRC UGENINI KUFUZU AFCON  MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Kalala Mayele usiku wa jana ameifungia bao la pili Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Gabón katika mchezo wa Kundi I kufuzu Fainali za Kombe la Matafa ya Afrika Uwanja wa Franceville nchini humo.
  Mayele alifunga bao hilo dakika ya 83 baada ya kumtoka beki wa Gabón na kufumua shuti lililomshinda kipa Jean-Noël Amonome, huku bao la kwanza la DRC likifungwa na mshambuliaji wa AEL ya 
  Cyprus, Aaron Tshibola dakika ya 34.
  Fiston Kalala Mayele mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho Afrika, alifunga baada ya kutokea benchi dakika ya 74 kuchukua nafasi ya Yoane Wissa wa Brentford ya England.
  Kwa ushindi huo DRC inafikisha pointi saba na kupanda kileleni mwa Kundi I ikiizidi tu wastani wa mabao Gabón, wakifuatiwa na Sudan pointi sita na Mauritania pointi tano baada ya wote kucheza mechi tano.
  Mechi za mwisho Septemba 4, DRC watakuwa wenyeji wa Sudan na Gabon watakuwa wageni wa Mauritania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE ATOKEA BENCHI KUIFUNGIA DRC UGENINI KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top