• HABARI MPYA

  Monday, June 19, 2023

  NI HISPANIA MABINGWA WA UEFA NATIONS LEAGUE 2022-2023


  HISPANIA wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa UEFA Nations League kwa ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Croatia baada ya sare ya bila kufungana, 0-0 usiku wa jana Uwanja wa Feijenoord Jijini Rotterdam nchini Uholanzi.
  Waliofunga penalti za Hispania ni Joselu, Rodri, Mikel Merino, Marco Asensio na Dani Carvajal, huku Aymeric Laporte akikosa wakati za Croatia zilifungwa na Nikola Vlašić, Marcelo Brozović, Luka Modrić na Ivan Perišić huku Lovro Majer na Bruno Petković wakikosa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI HISPANIA MABINGWA WA UEFA NATIONS LEAGUE 2022-2023 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top