• HABARI MPYA

  Tuesday, June 13, 2023

  MBEYA CITY YAICHAPA KMC 2-1 SOKOINE KUWANIA KUBAKI LIGI KUU


  TIMU ya Mbeya City imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kubaki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Gasper Mwaipasi dakika ya na tatu na Sixtus Sabilo kwa penalti dakika ya 37, wakati la KMC limefungwa na Abdul Hillary dakika ya 89.
  Timu hizo zitarudiana Ijumaa Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga na mshindi wa jumla atabaki Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kujaribu tena bahati ya kubaki ya Ligi Kuu kwa kumenyana na Mashujaa ya Kigoma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAICHAPA KMC 2-1 SOKOINE KUWANIA KUBAKI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top