• HABARI MPYA

  Thursday, June 15, 2023

  AMROUCHE ATAJA KIKOSI CHA STARS DHIDI YA NIGER JUMAPILI


  KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Mualgeria Adel Amrouche ametaja kikosi cha wachezaji 30 cha Taifa Stars kilichopo kambini Jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Niger Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023.
  Kuelekea mchezo huo wa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam ambao Taifa Stars itamkosa kipa wake namba moja, Aishi Manula ambaye ni majeruhi, Amrouche amewachukua makipa wasiadizi, Metacha Mnata wa Yanga na Benno Kakolanya wa Simba SC.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMROUCHE ATAJA KIKOSI CHA STARS DHIDI YA NIGER JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top