MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Kalala Mayele akiwa na kocha Mtunisia, Nasredine Mohamed Nabi baada ya kukutana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam leo.
Nabi anaondoka nchini kurejea kwao, Tunisia baada ya kuacha kazi Yanga kufuatia misimu miwili na nusu ya kufanya kazi Jangwani, wakati Mayele ndio anarejea nchini kutoka kuichezea timu yake ya taifa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Juzi Mayele aliifungia DRC bao la pili ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Gabón katika mchezo wa Kundi I kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Franceville nchini humo.
Mayele ambaye kwa sasa anaishi na familia yake nchini, amepokewa na mkewe na watoto wao ambao walikwenda na Tuzo alizoshinda akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa, ambazo ni Mchezaji Bora, Mfungaji Bora na Bao Bora katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
0 comments:
Post a Comment