KLABU ya Azam FC imeachana na aliyekuwa Kaimu kocha wake Mkuu, Muingereza mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kalimangonga Ongala.
Ongala anakuwa kocha wa tatu kuondolewa kazini baada ya Kocha wa makipa Mspaniola Dani Cadena na kocha wa Fiziki, Mtunisia Dk. Moadh Hiraoui.
Makocha hao wanaondoka kupisha wasaidizi wapya watakaoletwa na kocha mpya, Msenegal Youssouph Dabo ambaye ataanza kukiandaa kikosi kwa ajili ya msimu ujao.
Tayari Azam FC imeachana na wachezaji watano, ambao ni beki Mzimbabwe Bruce Kangwa, kiungo Mkenya, Kenneth Muguna na mshambuliaji Mzambia, Rodgers Kola na wazawa Ismail Aziz na Cleophace Mkandala.
0 comments:
Post a Comment