• HABARI MPYA

  Sunday, June 18, 2023

  TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI YA KUFUZU AFCON BAADA YA KUICHAPA NIGER 1-0  TANZANIA imeweka hai matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Ivory Coast baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger katika mchezo wa Kundi F leo Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao pekee la Taifa Stars, mshambuliaji wa Al-Qadsiah ya Saudi Arabia , Simon Happygod Msuva dakika ya 69 akimalizia krosi ya kiungo wa Zulte Waregem ya Ubelgiji, Novatus Dismass.
  Kwa ushindi huo, Taifa Stars inafikisha pointi katika mchezo wa tano saba na kupanda nafasi ya pili, nyuma ya Algeria yenye pointi 12 ambayo tayari imekwishafuzu.
  Algeria hivi sasa iko dimbani Uwanja wa Omnisport Jijini Douala nchini Cameroon ikimenyana na wenyeji, wahamiaji Uganda katika mchezo wa tano kwa wote.
  Uganda inaingia kwenye mchezo huo ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi zake nne mbele ya Niger yenye pointi mbili. Ikumbukwe Uganda itamalizia ugenini na Niger na Taifa Stars itaifuata Algeria Jijini Algiers.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI YA KUFUZU AFCON BAADA YA KUICHAPA NIGER 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top