UONGOZI wa klabu ya Yanga umetangaza kuachana na kocha wake Nasredeen Mohamed Nabi kufuatia Mtunisia huyo kukataa kuongeza mkataba baada ya kumaliza.
Nabi hakushinda taji katika msimu wake wa kwanza tu Yanga, lakini miwili iliyofuatia alibeba mataji yote, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Na msimu huu amewaaga vizuri Wananchi kwa kuwafikisha pia na Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambako walishindwa na USM Alger kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2, wakifungwa 2-1 Dar es Salaam na kushinda 1-0 Algiers.
0 comments:
Post a Comment