• HABARI MPYA

  Wednesday, June 28, 2023

  AZAM FC YASAJILI MCHEZAJI KUTOKA RAJA CASABLANCA


  KLABU ya Azam FC imemtambulisha kiungo wa Kimataifa wa Gambia,  Gibril Sillah kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao baada ya kufikia makubaliano na klabu yake, Raja Club Athletic ya Morocco.
  “Tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumefikia makubaliano na klabu ya Raja AC ya kumnunua kiungo wao mshambuliaji Gybrill Sillah,” imesema taarifa ya Azam.
  Nyota huyo wa Gambia, anatarajiwa kutua nchini muda wowote kuanzia sasa kumalizia taratibu za mwisho za usajili.
  Msimu uliopita kwenye Ligi Kuu ya Morocco, Sillah alifanikiwa kufunga jumla ya mabao saba na kutoa pasi za mwisho nne, wakati akiwa kwa mkopo JS Soualem.
  Huyo anakuwa mchezaji mpya wa pili tu Azam FC baada ya kiungo mwingine, Feisal Salum Abdallah kutoka Yanga SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI MCHEZAJI KUTOKA RAJA CASABLANCA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top