• HABARI MPYA

    Monday, June 19, 2023

    MASHUJAA FC YAICHAPA MBEYA CITY 3-1 KIGOMA


    TIMU ya Mashujaa ya Kigoma imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kupanda Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
    Mabao ya Mashujaa yamefungwa na Abihud Mtumbuka dakika ya 24, Asanga Stallone dakika ya 69 na Shadrack Ntabindi kwa penalti dakika ya 78, wakati la Mbeya City alijifunga Aziz Sibo dakika ya 63.
    Timu hizo zitarudiana Alhamisi Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya na Mbeya City itatakiwa kushinda 2-0 ili kufuzu kwa sheria ya mabao ya ugenini.
    Mshindi wa jumla atapanda Ligi Kuu na timu itakayofungwa itakwenda kucheza Ligi ya Championship. Ikumbukwe Mashujaa inacheza mchujo huu ikitoka Championship na Mbeya City imetoka Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MASHUJAA FC YAICHAPA MBEYA CITY 3-1 KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top