• HABARI MPYA

  Wednesday, June 21, 2023

  MTIBWA SUGAR YAANZA NA MOTO LIGI YA VIJANA U20


  MABINGWA watetezi, Mtibwa Sugar wameanza vyema Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Ezekiel Eusebio mawili, Athumani Makambo, Said Salum na Said Mkopi.
  Mechi nyingine ya Kundi A leo Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 3-1  dhidi ya Namungo FC hapo hapo, huku mechi za Kundi C Geita Gold ikiilaza KMC 2-0 na Coastal Unión ikiichapa Singida Big Stars 1-0 hapo hapo Chamazi.
  Kesho ni mechi za Kundi B Polisi na Tanzania Prisons Saa 8:00 mchana, Yanga na Dodoma Jiji Saa 10:15 jioni na za Kundi D Simba na Kagera Sugar Saa 12:30 jioni na Azam FC na Ihefu Saa 2:45 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAANZA NA MOTO LIGI YA VIJANA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top