NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma leo Juni 15, 2023 mkoani Tabora amefungua mashindano ya michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSSETA) kitaifa katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo Mhe. Mwinjuma amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya michezo nchini kwa kuanza na shule 56 za sekondari, mbili katika kila Mkoa, ili kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali
‘’Ndugu viongozi na wanamichezo Serikali kwa upande wake kupitia ushirikiano wa Wizara zetu tatu (Ya kwangu Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na TAMISEMI) imefanya jitihada kubwa katika kuimarisha shughuli za michezo katika shule za Msingi na Sekondari”amesema Mhe. Mwinjuma.
Mashindano hayo yatafanyika kwa siku saba yakihusisha timu za michezo mbalimbali kutoka Mikoa 32 ya Tanzania bara na Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment