• HABARI MPYA

  Friday, June 09, 2023

  MAYELE AFUNGANA KWA MABAO NA NTIBANZOKIZA


  MSHAMBULIAJI Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele amefungana kwa mabao na kiungo Mrundi wa Simba, Saido Ntibanzokiza katika kilele cha ufungaji Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
  Ntibanzokiza amezinduka katika mechi mbili za mwisho na kufunga mabao saba, huku Mayele akifunga moja zadi kwenye mchezo mmoja na wote sasa wana mabao 17.
  Kanuni za Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TBLB) haina kanuni inayoeleza kama wachezaji wakifungana kwa mabao kigezo kipi kitatumika kutoa tuzo hiyo.
  Lakini mara ya mwisho msimu wa 2016-2017 akiwa Yanga, Simon Msuva alifunga mabao 14, sawa na Abrahaman Mussa wa Ruvu Shooting na wawili hao wakapewa wote tuzo hiyo.
  Sherehe za utoaji zawadi za washindi wa Ligi Kuu zitafanyika Jumatatu mjini Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE AFUNGANA KWA MABAO NA NTIBANZOKIZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top