• HABARI MPYA

  Sunday, June 11, 2023

  YANGA KUWAKOSA AZIZ KI NA MAYELE MECHI NA AZAM KESHO


  KLABU ya Yanga itawakosa nyota wake wawili, kiungo Stephane Aziz Ki na mshambuliaji Fiston Kalala Mayele katika mchezo wa kesho wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Azam FC Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Wawili hao wameondoka leo Jijini Dar es Salaam kwenda kujiunga na timu zao za taifa, Mayele Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Aziz Ki Burkina Faso kwa ajili za wiki ijayo.
  Kocha wa Yanga, Nasredeen Nabi amesema walijaribu kuwaombea wachezaji bao wacheze ndio waondoke, lakini uongozi wa vyama vya Soka vya nchi zao umekatataa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUWAKOSA AZIZ KI NA MAYELE MECHI NA AZAM KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top