• HABARI MPYA

  Monday, June 12, 2023

  YANGA WAICHAPA AZAM FC 1-0 NA KUBEBA KOMBE LINGINE TANGA


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga wamefanikiwa kutetea mataji yote baada ya jioni hii kutwaa pia na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Shujaa wa Yanga leo ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Kennedy Musonda aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 14 akimalizia kazi nzuri ya beki Mkongo, Djuma Shabani.
  Pamoja na ubingwa wa Ligi Kuu na ASFC, Yanga pia ni washindi wa Ngao ya Jamii na washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika, wakihitimisha msimu mzuri kwao kihistoria chini ya kocha Mtunisia, Nasredeen Nabi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WAICHAPA AZAM FC 1-0 NA KUBEBA KOMBE LINGINE TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top