• HABARI MPYA

  Thursday, June 22, 2023

  JAMES AKAMINKO AONGEZA MKATABA AZAM FC HADI MWAKA 2026


  KIUNGO Mghana, James Akaminko ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea na kazi Azam FC hadi mwaka 2026.
  Taarifa ya Azam FC jioni hii imesema; “Kiungo chuma, James Akaminko, ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia ndani ya klabu yetu. Hivyo, bado yupo yupo sana kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2026,”.
  Akaminko alijiunga na Azam FC Julai mwaka jana akitokea Great Olympic ya kwao, baada ya awali kuchezea
  Pure Joy Stars, Tema Youth, Medeama na Ashanti Gold za kwao pia na US Tataouine ya Tunisia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JAMES AKAMINKO AONGEZA MKATABA AZAM FC HADI MWAKA 2026 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top