• HABARI MPYA

    Wednesday, June 14, 2023

    AZAM FC YAWAACHA KANGWA, MUGUNA NA RODGERS KOLA


    KLABU ya Azam FC imeachana na nyota wake watatu wa kigeni, beki Mzimbabwe Bruce Kangwa, kiungo Mkenya, Kenneth Muguna na mshambuliaji Mzambia, Rodgers Kola.
    Taarifa ya Azam FC kuachana na wachezaji hao imetoka muda mfupi baada ya taarifa ya awali ya kuwaondoa makocha wake wawili, Kocha wa makipa Mspaniola Dani Cadena na kocha wa Fiziki, Mtunisia Dk. Moadh Hiraoui.
    Makocha hao wanaondoka kupisha wasaidizi wapya watanaoletwa na kocha mpya, Msenegal Youssouph Dabo ambaye ataanza kukiandaa kikosi kwa ajili ya msimu ujao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAWAACHA KANGWA, MUGUNA NA RODGERS KOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top