• HABARI MPYA

  Friday, June 30, 2023

  NI MTIBWA NA GEITA GOLD FAINALI LIGI YA VIJANA U20


  TIMU za Mtibwa Sugar na Geita Gold zimefanikiwa kwenda Fainali ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya kuzitoa Azam FC na Kagera Sugar leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Katika Nusu Fainali ya kwanza Geita Gold imeichapa Kagera Sugar 2-0, mabao ya Saluja Mhoja na Frank Maganga na Nusu Fainali ya pili Mtibwa Sugar ikailaza Azam FC 2-1.
  Mabao yote ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Athumani Makambo huku la Azam FC likifungwa na David Chiwalanga.
  Fainali itapigwa Jumapili hapo hapo a Chamazi ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu katí ya Kagera Sugar na Azam FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI MTIBWA NA GEITA GOLD FAINALI LIGI YA VIJANA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top