• HABARI MPYA

  Friday, June 23, 2023

  MTIBWA SUGAR YAENDELEZA UBABE LIGI YA VIJANA U20


  MABINGWA watetezi, Mtibwa Sugar wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Athumani Makambo mawili na Ezekiel Zenobi moja na huo ukiwa ushindi wa pili mfululizo baada ya kuichapa Mbeya City 5-0 kwenye mchezo wa kwanza.
  Mechi nyingine ya Kundi A leo Mbeya City imeshinda 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting, wakati mechi za Kundi C Geita Gold wameiltandika Singida Big Stars 3-1 na Coastal Unión imeilaza KMC 1-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAENDELEZA UBABE LIGI YA VIJANA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top