MFANYABIASHARA, Mwanasiasa na Mfadhili wa zamani wa michezo visiwani Zanzibar, Mohamed Raza Hassanali Dharamsi amefariki dunia leo Jijini Dar es Salaam akiwa ana umri wa miaka 60.
Kwa mujibu wa taarifa, Raza aliyewahi kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, Kusini Unguja amezikwa jioni ya leo katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.
Enzi za uhai wake, Raza alikuwa mmoja wafadhili maarufu wa michezo Zanzibar na alikuwa pia akiisaidia klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment