• HABARI MPYA

    Thursday, June 22, 2023

    HISTORIA YA BENO KAKOLANYA SIMBA SC YAFUNGWA RASMI


    HATIMAYE klabu imeachana na mlinda mlango Beno David Kakolanya baada ya miaka minne ya kuwa naye tangu awasili kutoka kwa mahasimu, Yanga SC.
    “Hatutaendelea kuwa na mlinda mlango, Beno Kakolanya baada ya mkataba wake kumalizika,”imesema taarifa ya Simba SC mchana wa leo.
    Kakolanya anakuwa mchezaji wa tano kuachwa Simba baada ya beki Muivory Coast, Mohamed Ouattara, na viungo Wanigeria, Nelson Okwa, Víctor Akpan na Mghana, Augustine Okrah.
    Simba pia imeachana na makocha wake wawili wa Fiziki, Kelvin Mandla Ndlomo na Fareed Cassiem, wote raia wa Afrika Kusini na kocha wa makipa, Mmorocco, Zakaria Chlouha na kocha wake wa timu yake ya wanawake, Mganda Charles Lukula.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HISTORIA YA BENO KAKOLANYA SIMBA SC YAFUNGWA RASMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top