• HABARI MPYA

  Friday, June 23, 2023

  SIMBA SC YAACHANA NA GARDIEL MICHAEL BAADA YA MIAKA MINNE


  KLABU ya Simba imetangaza kuachana na beki wa kushoto, Gardiel Michael Mbaga baada ya miaka minne ya kupiga kazi Msimbazi tangu Julai 2019 aliposajiliwa kutoka kwa watani, Yanga.
  “Uongozi wa klabu unapenda kuwajulisha kuwa hatutaendelea kuwa na mlinzi wa kushoto Gadiel Michael baada ya mkataba wake kufikia tamati,” imesema taarifa ya Simba mchana huu.
  Gardiel Michael anakuwa mchezaji wa saba kuachwa Simba baada ya kipa Beno Kakolanya, beki Muivory Coast, Mohamed Ouattara, na viungo Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Wanigeria, Nelson Okwa, Víctor Akpan na Mghana, Augustine Okrah.
  Simba pia imeachana na makocha wake wawili wa Fiziki, Kelvin Mandla Ndlomo na Fareed Cassiem, wote raia wa Afrika Kusini na kocha wa makipa, Mmorocco, Zakaria Chlouha na kocha wake wa timu yake ya wanawake, Mganda Charles Lukula.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAACHANA NA GARDIEL MICHAEL BAADA YA MIAKA MINNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top