• HABARI MPYA

    Thursday, June 22, 2023

    SIMBA SC YAACHANA NA MCHEZAJI KIRAKA ERASTO NYONI


    KLABU ya Simba imetangaza kuachana na kiungo mkongwe anayeweza kucheza nafasi zote za ulinzi katikati na pembeni, Erasto Edward Nyoni baada ya kuitumikia timu tangu mwaka 2017 aliposajiliwa kutoka Azam FC.
    Erasto Nyoni anakuwa mchezaji wa sita kuachwa Simba baada ya kipa Beno Kakolanya, beki Muivory Coast, Mohamed Ouattara, na viungo Wanigeria, Nelson Okwa, Víctor Akpan na Mghana, Augustine Okrah.
    Simba pia imeachana na makocha wake wawili wa Fiziki, Kelvin Mandla Ndlomo na Fareed Cassiem, wote raia wa Afrika Kusini na kocha wa makipa, Mmorocco, Zakaria Chlouha na kocha wake wa timu yake ya wanawake, Mganda Charles Lukula.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAACHANA NA MCHEZAJI KIRAKA ERASTO NYONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top