REFA Ramadhani Kayoko ndiye atakayepuliza kipyenga katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kesho baina ya Azam na Yanga Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Kayoko wa Dar es Salaam atasaidiwa na mwenyeji, Mohamed Mkono na Janeth Balama wa Iringa, wakati refa wa akiba na Jonesia Rukyaa wa Kagera.
Mchezo huo utaanza Saa 9:30 Alasiri na kuonyeshwa na chaneli ya Azam Sports 1 HD ya Azam Tv.
0 comments:
Post a Comment