KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Yakubu, amesema Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) katika sekta ya michezo nchini ili kuendelea kutoa ajira kwa watu wengi zaidi hatua inayosaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Yakubu amesema katika kikao chake na Mtaalamu wa michezo kutoka Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) Dkt. Shiraishi Tomoya Juni 01, 2023 jijini Dodoma.
“Uwepo wako hapa nchini utasaidia wananchi kuongeza hamasa ya michezo na watu wengi wakishiriki watakwepa magonjwa yasiyoambukiza, Rais yuko mstari wa mbele katika michezo, naamini uwepo wako hapa nchini utasaidia kukuza michezo na kuifanya kuwa maarufu na watu wengi kushiriki” amesema Yakubu.
Kwa upande wake Dkt. Shiraishi Tomoya amesema ana uzoefu wa nchi za Afrika Mashariki na anaiona michezo katika miaka 10 ijayo michezo inakuwa sehemu ya jamii ambapo watu wote watashiriki na kuimarisha afya zao.
Dkt. Shiraishi Tomoya ni mtaalamu na mshauri wa michezo na maendeleo atakuwepo nchini na kufanya kazi katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na atakuwa nchini kwa muda wa miaka mitatu kutoka 2023 hadi 2027.
0 comments:
Post a Comment