• HABARI MPYA

    Saturday, June 24, 2023

    WAZIRI WA MICHEZO DK. PINDI CHANA AITA WAWEKEZAJI KWENYE NETIBOLI


    WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewakaribisha wadau na wapenda michezo wa sekta binafsi wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika shughuli za michezo hususani mchezo wa Netiboli.
    Mhe. Chana amesema hayo Juni 23, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mashindano ya Klabu Bingwa ya Netiboli katika viwanja vya Netiboli, Benjamini Mkapa.
    “Nitoe wito kwa wadau wengine zikiwemo taasisi mbalimbali za ndani na nje kuwekeza katika michezo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya kimichezo Pamoja na kugharamia shughuli za michezo hususani michezo ya wanawake pamoja na watu wenye ulemavu” amesema Mhe. Chana
    Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Dkt. Devota Marwa amesema kuwa wataendelea kuratibu programu mbalimbali za maendeleo ya mchezo huo.
    Mashindano hayo yamelenga kuchochea ushindani na kupata timu bora ya taifa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI WA MICHEZO DK. PINDI CHANA AITA WAWEKEZAJI KWENYE NETIBOLI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top