• HABARI MPYA

    Friday, March 10, 2023

    RUVU SHOOTING YAICHAPA MBEYA CITY 2-1 SOKOINE

     


    TIMU ya Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Mabao ya Ruvu Shooting katika mchezo huo yamefungwa na Valentino Mashaka dakika ya 30 na Abrahman Mussa dakika ya 81, wakati la Mbeya City limefungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 41 kwa penalti.
    Kwa ushindi huo, Ruvu Shooting inafikisha pointi 20 na kusogea nafasi ya 15, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake 27 nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 25.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAICHAPA MBEYA CITY 2-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top