• HABARI MPYA

  Saturday, March 04, 2023

  MAN CITY YAIFUMUA NEWCASTLE UNITED 2-0 ETIHAD


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Phil Foden dakika ya 15 na super-sub Bernardo Silva dakika ya 67 na kwa ushindi huo, kikosi cha Pep Guardiola kinafikisha pointi 58 katika mchezo wa 26, ingawa kinabaki nafasi ya pili kikizidiwa pointi mbili na Arsenal yenye mechi 25.
  Kwa upande wao, Newcastle United baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 41 za mechi 24 nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIFUMUA NEWCASTLE UNITED 2-0 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top