• HABARI MPYA

  Saturday, March 04, 2023

  DUCHU AIPELEKA MTIBWA SUGAR NANE BORA ASFC


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya KMC leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Bao pekee la Mtibwa Sugar leo limefungwa na beki wake wa kulia, David Kameta ‘Duchu’ kwa mkwaju wa penalti dakika ya 45 baada ya mlinzi wa KMC kuunawa mpira kwenye boksi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DUCHU AIPELEKA MTIBWA SUGAR NANE BORA ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top