• HABARI MPYA

    Sunday, March 12, 2023

    ARSENAL MOTO BATÍ, YASHINDA 3-0 UGENINI


    VINARA, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.
    Mabao ya Arsenal yamefungwa na Gabriel Magalhães dakika ya 21, Gabriel Martinelli dakika ya 26 na Martin Odegaard dakika ya 45.
    Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 66 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City kufuatia wote kucheza mechi 27, wakati Fulham inabaki na pointi zake 39 za mechi 27 pia nafasi ya nane.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL MOTO BATÍ, YASHINDA 3-0 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top