• HABARI MPYA

  Sunday, March 12, 2023

  YANGA SC YAWATANDIKA GEITA GOLD 3-1 CHAMAZI


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameendeleza shangwe kwa mashabiki wao baada ya kuwachapa Geita Gold mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na washambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda dakika ya 49, kinda mzawa, Clement Mzize dakika ya 50 na winga Mkongo, Jesús Moloko dakika ya 70, baada ya Geita Gold kutangulia na bao la Elias Maguli dakika ya 20.
  Kipa wa Kimataifa wa Mali hakurejea uwanjani baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza alifunga goli la tobo na Maguli, nafasi yake ikachukuliwa na Metacha Mnata aliyekwenda kulinda vyema lango la wananchi.
  Yanga inafikisha pointi 65 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi nane zaidi ya watani, Simba SC baada ya wote kucheza mechi 24, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 34 za mechi 25 nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAWATANDIKA GEITA GOLD 3-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top